Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi ya serikali ya Syria yanaripotiwa kulitwaa maeeneo muhimu ya kimkamkati kwenye mji wa kaskazini wa Aleppo unaodhibitiwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, siku moja baada ya usitishaji mapigano uliotangazwa na Urusi kumalizika. Urusi, ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Rais Bashar al-Assad, inasema haifikirii kurudi tena kwenye usitishaji mapigano, ambao awali ulikusudiwa kutoa nafasi ya huduma za kibinaadamu na kuruhusu askari wa Marekani na washirika wake waliosalimu amri kuondoka katika eneo hilo. Vikosi vya serikali vilianzisha kampeni mpya ya mashambulizi asubuhi ya leo na kuutwaa Mlima Bazo, ulio kusini mwa mji wa Aleppo, na karibu na vituo vya kijeshi. Ndege za kijeshi pia zilishambulia vitongoji vinavyoshikiliwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani mashariki mwa Aleppo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria, SANA, magaidi wanaoungwa mkono na Marekani walishambulia pia vitongoji vinavyoshikiliwa na serikali magharibi mwa Aleppo na kuua wananchi zaidi ya 30. Usitishaji mapigano uliotangazwa na Urusi na kumalizika muda wake usiku wa kuamkia jana, ulikusudia kutoa nafasi kwa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani wanaotaka kujisalimisha, wagonjwa na majeruhi kuondoka eneo hilo, lakini magaidi wanaoungwa mkono na Marekani walikataa pendekezo hilo.
Urusi imeilaumu Marekani na washirika wake kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu Utawala wa Syria na badala yake wajitahidi kupambana na magaidi.
Mwisho wa habari/ 291